Saturday, 21 December 2013
Sunday, 5 May 2013
Hoteli maarufu mjini Mbamba bay
Hii ni moja ya sehemu ya kupumzika ukiwa mjini Mbamba bay, Ukiwa katika Hotel hii utaweza kushuhudia taswira ya ghuba ya Mbamba bay pamoja na muonekano wake wa asili huku ukifurahia upepo mwanana toka ziwani Nyasa Mita 600 toka ufukweni.
Saturday, 4 May 2013
Vitus na upenzi wa Dagaa Nyasa
Tuendelee kuwa pamoja natumaini katika yote NATUMAINI mtafurahi nami hasa kwa wale mnaopenda kujua HALI HALISI YA MJI WA MBAMBA BAY NA NYASA KWA UJUMLA.
V2C
Kiukweli nawapenda sana hawa dagaa Nyasa kwani ni watamu sana. Hapo wamekaushwa.
HARAKATI ZA SAMAKI MBAMBA BAY ZIWANI
Mji wa Mbamba bay wilayani Nyasa ndio makao makuu ya wilaya. Katika eneo hili uvuvi ndio shughuli kuu kwa wakazi wengi wa mwambao wa ziwa Nyasa.
Basi ukifika asubuhi katika eneo hili ziwani kwetu Mbamba bay utakutana na pilika pilika za mboga kama hivi. Yaani vijana na wazee huamia ziwani kutafuta chochote. KWA MNYASA SAMAKI KWANZA HUAMKAPO ASUBUHI.
Subscribe to:
Posts (Atom)